Updated Thursday, July 28, 2016

Ndege kubwa zaidi inayotumia nishati ya jua yamaliza safari yake ya kuzunguka dunia


Ndege kubwa zaidi inayotumia nishati ya jua Solar Impulse 2 ilitua tarehe 26 alfajiri kwenye uwanja wa ndege wa Al Bateen, mjini Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu, na kumaliza safari yake ya kilomita elfu 35 duniani. Safari hii imeweka rekodi ya safari ya ndege ya kuzunguka dunia inayotegemea nishati ya jua tu.

Kabla ya hapo, tarehe 24 alfajiri ndege hiyo iliruka katika uwanja wa ndege wa kimataifa mjini Cairo, Misri, na kuanza kipindi cha mwisho cha safari yake.

Ndege hii iliyosanifiwa na kampuni ya Uswisi, inaweza kuruka siku nzima kwa kutegemea nishati ya jua tu. Upana wa mabawa ya ndege hiyo ni mita 72, ambao ni mrefu zaidi kuliko ndege ya abiria ya Boeing 747. Kwenye mabawa hayo kuna betri zaidi ya elfu 17 za nishati ya jua, na nishati ya ziada inayozalishwa mchana inahifadhiwa kwenye betri za Li-ion ili itumiwe wakati wa usiku.

Bw Bertrand Piccard na Bw. Andre Borschberg kutoka Uswisi waliendesha ndege hiyo kwa zamu. Mwezi Machi mwaka jana, ndege hiyo ilifunga safari mjini Abu Dhabi, na kuanza safari yake ya kuzunguka dunia, ikitangaza umuhimu wa matumizi ya nishati safi. Njiani ilitua katika miji 16 ya nchi mbalimbali zikiwemo Aman, India, Myammar, China, Japan, Marekani, Hispania na Misri.
Ndege kubwa zaidi inayotumia nishati ya jua yamaliza safari yake ya kuzunguka dunia Ndege kubwa zaidi inayotumia nishati ya jua yamaliza safari yake ya kuzunguka dunia Reviewed by Bill Bright Williams on 1:17:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.