Updated Thursday, July 7, 2016

Messi ahukumiwa kifungo cha miezi 21 kwa madai ya ukwepaji ushuru


Mahakama ya Barcelona yatoa hukumu ya kifungo cha miezi 21 kwa Lionel Messi na babake Jorge Horacio Messi.
Mahakama ya Barcelona imetoa hukumu ya kifungo cha miezi 21 dhidi ya Lionel Messi na babake Jorge Horacio Messi kwa madai ya ukwepaji ushuru.
Messi na baba yake, Jorge Horacio Messi, walipatikana na hatia ya kukwepa kodi nchini Hispania kiasi cha € 4,100,000 ($ 4,500,000) kati ya mwaka 2007 na '09.
Enrique Bacigalupo na Javier Sanchez ambao ni mawakili wa Messi na babake, wametoa maelezo na kuharifu kwamba watawasilisha kesi hiyo katika Mahakama kuu ya Uhispania ili kupinga hukumu hiyo.

Mawakili hao wanatarajia kusikilizwa na mahakama kuu ili iweze kutoa uamuzi wake ndani ya kipindi cha chini ya mwaka mmoja.

Mawakili hao pia wamesisitiza kwamba bado wanayo matumaini ya kufutiliwa mbali kwa hukumu hiyo dhidi ya Messi na babake.

Kwa upande mwengine, klabu ya Barcelona imetoa maelezo na kufahamisha kwamba itaendelea kusimama bega kwa bega na Messi pamoja na familia yake kwa ujumla.
Messi ahukumiwa kifungo cha miezi 21 kwa madai ya ukwepaji ushuru Messi ahukumiwa kifungo cha miezi 21 kwa madai ya ukwepaji ushuru Reviewed by Bill Bright Williams on 1:20:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.