Updated Monday, July 4, 2016

Maumivu ya sehemu ya chini ya mgongo


Maumivu ya sehemu ya chini ya mgongo au lumbago ni hali inayotokea mara nyingi kwenye hali inayohusu misuli na mifupa ya mgongo. 
Hali hii huathiri takriban 40% ya watu kwa wakati fulani maishani mwao. Maumivu ya sehemu ya chini ya mgongo yanaweza kuainishwa kwa urefu kama maumivu makali ya ghafla (yanayodumu kwa kipindi cha chini ya wiki 6), maumivu sugu ya wastani (wiki 6 hadi 12), au maumivu sugu (zaidi ya wiki 12). 
Hali hii pia inaweza kuainishwa kulingana na visababishi kama inayosababishwa na jeraha au isiyosababishwa na jeraha au maumivu hame .
Maumivu haya usikika na kuumiza pale unapoinua kitu, kusimama, kukaa kwenye kiti au kutembea na usababishwa na matumizi kupita kiasi ya misuli, kano, mishipa na neva za mgongoni au kwenye pingili za uti wa mgongo kutokana na kugandamizwa sana. Pia huweza kusababishwa na kuvunjika au maambukizi katika pingili za uti wa mgongo, umri mkubwa, saratani ya mifupa,uzito kupita kiasi mawe katika figo, uvimbe na saratani ya kizazi .

Matibabu ya maumivu ya ghafla ya mgongo kwa kawaida huwa ni tiba isiyohusisha upasuaji, kama vile vituliza maumivu na kuendeleza kazi za kawaida jinsi mtu anavyoweza licha ya maumivu. Matibabu hupendekezwa kwa kipindi ambapo yanamsaidia mtu, huku dawa aina ya acetaminophen (pia inayojulikana kama paracetamol) ikiwa ya kwanza kupendekezwa.

TIBA YA MAUMIVU CHINI YA MGONGO
Unaweza kujifanyia huduma ya kwanza mwenye kwa kutumia dawa za kupunguza maumivu, kuchua, kuweka barafu au joto kiasi, kufanya mazoezi mapesi nakukaa au kulala mtindo unaopunguza maumivu.
Punguza uzito, epuka kuanguka mara kwa mara na usibebe mizigo mizito kupita kiasi au kaza sana tumbo unaponyanyua mizigo mizito
Usizunguke wakati au kuinamia mbele wakati umebeba vitu vizito
Usisimame kwa kubana miguu muda mrefu
Maumivu yakizidi fika hospitali ili kufanyiwa uchunguzi na vipimo vya X rays, CT scan na MRIs kwa ajili ya kugundua tatizo na kupata tiba zaidi.

Maumivu ya sehemu ya chini ya mgongo Maumivu ya sehemu ya chini ya mgongo Reviewed by Bill Bright Williams on 7:38:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.