Updated Wednesday, July 20, 2016

Marekani yatengeneza chombo cha uchunguzi wa sayari ya Mars kitakachorushwa mwaka 2020


Shirika la anga ya juu la Marekani NASA limetangaza kuwa chombo kipya cha uchunguzi wa sayari ya Mars kitakachorushwa mwaka 2020 kimeingia hatua ya mwisho ya usanifu na utengenezaji.

Kama kazi zote zitaendelea vizuri, chombo hiki kitarushwa katika majira ya joto ya mwaka 2020, kufika Mars mwezi Februari mwaka 2021, kutua kwenye sehemu iliyofaa kwa maisha ya viumbe vidogovidogo katika zama za kale, kuanza kazi ya kutafuta dalili ya kuwepo kwa viumbe kwenye sayari hiyo, na kukusanya sampuli za udongo na miamba, ili sampuli hizi ziletwe duniani baadaye.

Kaimu naibu mkuu wa NASA Bw. Geoffrey Yoder alisema kuleta sampuli hizi duniani kunahitaji hatua nyingi, na kutekeleza mradi wa kurusha chombo cha uchunguzi mwaka 2020 ni hatua ya kwanza.

Ili kupunguza hatari na gharama, chombo hiki kitasanifiwa na kutengenezwa kwa teknolojia inayofanana na chombo cha uchunguzi cha Curiosity, kwa mfano, vyombo hivi vyote vina magurudumu sita. Lakini chombo hiki kipya kitabeba vifaa vipya, na kufanya uchunguzi mpya, ukiwemo kuchunguza kama sayari ya Mars ina hewa ya Oxygen ya kutosha baada ya binadamu kufika kwenye sayari hii katika siku zijazo.

Lengo la mwisho la NASA ni kupeleka wanaanga kwenye sayari hiyo, lakini kwa mujibu wa mpango wa serikali, lengo hili halitatimizwa kabla ya mwaka 2030.
Marekani yatengeneza chombo cha uchunguzi wa sayari ya Mars kitakachorushwa mwaka 2020 Marekani yatengeneza chombo cha uchunguzi wa sayari ya Mars kitakachorushwa mwaka 2020 Reviewed by Bill Bright Williams on 3:34:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.