Updated Friday, July 1, 2016

Maelfu ya raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wakimbilia Chad


Imeripotiwa kuwa maelfu ya raia kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati wamekimbilia nchini Chad.
Duru za kuaminika zimetangaza kuwa maelfu ya raia toka Jamhuri ya Afrika ya Kati wanaendelea kuwasili Chad kwa ajili ya hifadhi ambapo wakimbizi hao wataishi  katika kambi za wakimbizi zilizoko katika eneo la Min la kusini magharibi mwa Chad. 

Wakimbizi zaidi ya elfu 64 wamepatiwa makazi katika maeneo ya kusini na kusini mashariki mwa Chad; huku wengi wakiishi katika kambi sita na wengine waliosalia wakiwa wamepatiwa hifadhi katika maeneo ya vijijini. Jamhuri ya Afrika ya Kati ilikumbwa na hali ya machafuko tangu mwaka 2013 baada ya kuzuka mapigano ya kikabila na kidini na kuangushwa serikali iliyokuwepo madarakani wakati huo ya François Bozizé. Weledi wengi wa mambo wanaamini kuwa serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati inapaswa kuchukua hatua madhubuti haraka iwezekanavyo na kusitisha mapigano na mizozo ya ndani kupitia kuongeza juhudi za kuwakidhia raia mahitaji yao ya kimsingi, kuandaa mazingira ya kurejea nchini wakimbizi na kuboresha hali ya uchumi wa nchi hiyo.

      
Maelfu ya raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wakimbilia Chad Maelfu ya raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wakimbilia Chad Reviewed by Bill Bright Williams on 11:29:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.