Updated Thursday, July 21, 2016

Maandano ya kumpinga Donald Trump yafanyika Marekani


Watu kadhaa wenye asili ya Hispania wamejitokeza na bango lililo mfano wa ukuta kumpinga mgombea urais wa chama cha Republican Donald Trump kwenye jimbo la Ohio nchini Marekani. Mkutano wa kitaifa wa chama hicho unafanyika jimboni humo.

Kundi la wahamiaji kutoka Mexico na mashirika mengine waliitisha mkutano huo. Takribani watu mia moja walikusanyika kwenye uwanja wa wazi jirani na mkutano huo huko Cleveland jana Jumatano asubuhi.

Washiriki waliokuwa wamebeba mabango wakiwa pamoja na mfano wa sehemu ya kuta waliandamana kuelekea kwenye ukumbi wa mkutano. Walisema kuwa ni bora ukuta ujengwe kumzunguka Trump.

Baadaye walizingira eneo la kuingilia kwenye ukumbi huo wakiwa wamebeba mfano wa ukuta wenye urefu wa zaidi ya mita mia moja. 

Ilani ya uchaguzi ya chama hicho iliidhinishwa kwenye siku ya kwanza ya mkutano huo Jumatatu iliyopita. Inatoa wito wa kujenga kuta kwenye eneo la kusini lililopo mkabala na mpaka wa Mexico. Trump anapigia chapuo sera hiyo.

Kijana mhamiaji kutoka Mexico mwenye umri wa miaka 28 alisema anataka Trump afikirie kwa makini juu ya hatua zake na maneno anayoyasema akiwa mtu anayekiwakilisha chama cha Republican na Marekani kwa ujumla.

Vyama vya kiraia vimekuwa vikifanya maandamano jirani na ukumbi kumpinga Trump. Idadi kubwa ya maafisa wa polisi imepelekwa kwenye eneo hilo.
Maandano ya kumpinga Donald Trump yafanyika Marekani Maandano ya kumpinga Donald Trump yafanyika Marekani Reviewed by Bill Bright Williams on 1:14:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.