Updated Friday, July 1, 2016

Kundi la watu waliojihami lashambulia msafara wa jeshi na kuwajeruhi wanajeshi 6 wa Mali


Wanajeshi 6 wameripotiwa kujeruhiwa baada ya msafara wao kushambuliwa na kundi la watu waliojihami katika eneo la Timbuktu lililoko kaskazini mwa Mali.

Mashambulizi hayo yalitekelezwa baada ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kutangaza kurefusha muda wa kuhudumu kwa kikosi cha MINUSMA hadi tarehe 30 Juni 2017.

Wakati huo huo, baraza hilo pia limetangaza mpango wa kuongeza idadi ya wanajeshi zaidi ya 2,000 kwa lengo la kuimarisha kikosi cha MINUSMA.

Nchi ya Mali imekuwa ikikumbwa na mashambulizi yanayotekelezwa mara kwa mara na makundi ya wapiganaji dhidi ya serikali tangu mwaka 2012.

Licha ya makundi hayo kutia saini mkataba wa amani mwezi Juni mwaka jana, bado mzozo umeonekana kuendelea nchini humo.

Takriban wanajeshi 90 wa kikosi cha MINUSMA wamepoteza maisha kwenye mashambulizi yaliyotekelezwa tangu mwaka 2013.

Kundi la watu waliojihami lashambulia msafara wa jeshi na kuwajeruhi wanajeshi 6 wa Mali Kundi la watu waliojihami lashambulia msafara wa jeshi na kuwajeruhi wanajeshi 6 wa Mali Reviewed by Bill Bright Williams on 9:06:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.