Updated Friday, July 1, 2016

Kinga dhidi ya virusi vya Zika kujaribiwa kwa binadamu


Kinga ambayo imepewa jina la SynCon Zika DNA vaccine (GLS-5700) imeonesha matokeo mazuri  baada ya kujaribiwa kwa wanyama wadogo na wakubwa.

Uongozi wa shirika linalohusika kuhusu chakula la dawa la Marekani  limefahamisha kutoa ruhusa ya kujaribu kinga dhidi ya Zika kwa binadamu.

Taarifa hiyo ilitolewa Jumatatu na kitengo hicho.

Kinga hiyo ambayo imepatikana kwa ushirikiano ya makampuni ya kutengeneza dawa Inovio Pharmaceuticals na GeneOne Life Science, kinga hiyo kwa jina la GLS-5700 imeripotiwa kutoa matumaini baada ya kujaribiwa kwa wanyama.
Dr. J. Joseph Kim, Mkurugenzi na mtendaji mkuu wa Inovio alisema,"tuna fahari kupata idhini ya kuanzisha chanjo ya Zika kwa baadhi ya watu kuwa tayari kujitolea kwa ajili ya utafiti.

Kinga hiyo ya majaribio itafanyika kwa watu 40 na matokea kutangazwa baada ya miezi kadhaa.
Kinga dhidi ya virusi vya Zika kujaribiwa kwa binadamu Kinga dhidi ya virusi vya Zika kujaribiwa kwa binadamu Reviewed by Bill Bright Williams on 1:26:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.