Updated Friday, July 1, 2016

Kampuni ya kinywaji cha 'Red Bull' yaomba radhi kwa Indonesia kwa kufanya tangazo la kukeraKampuni ya Red Bull imeomba msamaha kwa Indonesia kwa kutoa tangazo kuhusu kinywaji cha kampuni hiyo lilionyesha mwanariadha akifanya akrobatiki katika hekalu moja nchini humo ambalo linaaminika kuwa eneo takatifu.

Kampuni hiyo ilikubali kuwa ilitoa video hiyo bila ya kupata idhini kutoka mamlaka husika .
Video hiyo ya tangazo la Red Bull inaonyesha mwanariadha huyo akiruka katika vijiwe vya hekalu hiyo jambo ambalo lilizua hasira kutoka kwa raia wa Indonesia hasa upande wa Borobudur ambapo watu wengi ni wa dini ya kibuddha .

Tangazo hilo liliwekwa mtandaoni Machi 18, na kusababisha hasira huku serikali ya Indonesia ikitishia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya kampuni hiyo.

Hata hivyo mnamo mwezi Juni Red Bull ilikutana na viongozi wa serikali na kuahidi kuwa itaomba radhi rasmi Indonesia katika magazeti ya kitaifa .
Kampuni ya kinywaji cha 'Red Bull' yaomba radhi kwa Indonesia kwa kufanya tangazo la kukera Kampuni ya kinywaji cha 'Red Bull' yaomba radhi kwa Indonesia kwa kufanya tangazo la kukera Reviewed by Bill Bright Williams on 12:18:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.