Updated Friday, July 29, 2016

Clinton akubali uteuzi wake kwa uchaguzi wa urais


Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Democratic, Hillary Clinton, amekubali uteuzi wake kuwania kinyang'anyiro cha urais katika uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika Novemba 8 mwaka huu nchini Marekani.

"Ni kwa unyenyekevu na ujasiri ninaukubali uteuzi huu," amesema aliyekuwa Waziri wa Mashauriano ya Kigeni nchini Marekani Hillry Clinton, wakati wa hotuba rasmi katika mji wa Philadelphia Alhamisi Julai 28.

Hillary Clinton amewataka Wamarekani kukataa njia ya hofu inayotumiwa na Donald Trump, mgombea wa chama cha Republican. Bi Clinton ameahidi kukabiliana na changamoto moja baada ya nyingine, pamoja na kuweka kipaumbele kwa ajira.

Mgombea wa chama cha Democratic amejitokeza na kumshambulia kwa maneno makali mgombea mwenza, Donald Trump, ambaye, kwa mujibu wa Hillary Clinton, anataka kuiokoa nchi "peke yake". "Ninaweza kuweka sawa hali ya usalama ya Marekani, mimi mwenyewe, " amesema Bi Clinton, akibaini kwamba "haya yalikuwa maneno ya Donald Trump wakati alipokua akihutubia wajumbe wa chama cha Republican katika mji wa Cleveland [wakati wa makubaliano ya chama cha Republican]. Na maneno hayo lazima tuwe na wasiwasi sisi wote, " Hillary Clinton amesema.

Hillary Clinton alitoa ujumbe wa matumaini kwa Wamarekani wanaokabiliwa na mdororo wa kiuchumi na waathirika wa utandawazi. "Kazi yangu kubwa kama rais itakuwa kutoa fursa zaidi kwa ajira nzuri na kuongeza mishahara hapa nchini Marekani," Hillary Clinton aliongeza.
Clinton akubali uteuzi wake kwa uchaguzi wa urais Clinton akubali uteuzi wake kwa uchaguzi wa urais Reviewed by Bill Bright Williams on 12:28:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.