Updated Friday, July 1, 2016

Chuki dhidi ya wahajiri Uingereza zaongezeka baada ya Brexit


Chuki dhidi ya wahajiri nchini Uingereza zimeongezeka kwa asilimia kubwa, siku chache baada ya nchi hiyo kupiga kura ya kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya maarufu kama Brexit.

Baraza la Taifa la Polisi Uingereza (NPCC) limesema katika kipindi cha wiki moja iliyopita tangu nchi hiyo ijitoe EU, limerekodi kesi 330 zinazohusu jinai za chuki haswa dhidi ya wahajiri, ikilinganishwa na wastani wa kesi 63 kwa wiki hapo awali. Sara Thornton, mkuu wa baraza hilo amesema wameshangazwa sana na ongezeko hilo la chuki dhidi ya wahamiaji na hawaelewi lina mafungamano gani na hatua ya Uingereza kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya. Amesema kuwa baadhi ya jinai wanazofanyiwa wahajiri nchini humo ni pamoja na kupigwa, kutukanwa, kurushiwa vijikaratasi vyenye jumbe za kuwadhalilisha na kukejeliwa katika mitandao ya kijamii.

Haya yanajiri katika hali ambayo, chuki dhidi ya watu kutoka Asia nchini Uingereza pia imeripotiwa kuongezeka maradufu katika miezi ya hivi karibuni. 

      
Chuki dhidi ya wahajiri Uingereza zaongezeka baada ya Brexit Chuki dhidi ya wahajiri Uingereza zaongezeka baada ya Brexit Reviewed by Bill Bright Williams on 11:09:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.