Updated Thursday, July 21, 2016

China yaikopesha Serikali ya Tanzania Shilingi Trilioni 16


Benki ya Exim ya China imetoa mkopo wenye masharti nafuu wa dola za Marekani Bilioni 7.6  ikiwa ni zaidi ya Shilingi Trilioni 16 za Kitanzania kwa ajili ya kugharamia ujenzi wa mradi mkubwa wa reli ya kati  kwa kiwango cha kisasa  unaotarajiwa kuanza mwaka huu wa fedha.

Akipokea taarifa ya kukubaliwa kupewa fedha hizo mjini Dodoma Rais John Magufuli amesema  kutekelezwa kwa mradi huo kutasaidia kuinua uchumi wa Tanzania na nchi jirani zisizopakana na bahari zikiwemo Uganda, Rwanda, Burundi, na Congo.                         
Kwaupande wake Rais wa Benki ya Exim ya China  Liu Liang amempongeza Rais Magufuli na serikali yake kwa dhamira ya dhati ya kuiletea nchi hiyo maendeleo ikiwemo kuharakisha ujenzi wa reli ya kati na ameahidi kuwa benki yake itatoa ushirikiano wa karibu katika kufanikisha mradi huo na miradi mingine ya maendeleo.

Mradi wa ujenzi wa reli ya kati utahusisha ujenzi wa reli kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge) kutoka DAR ES SALAAM-TABORA-ISAKA-MWANZA, TABORA-MPANDA-KALEMELA, TABORA-UVINZA-KIGOMA NA ISAKA-KEZA-MSONGATI.
China yaikopesha Serikali ya Tanzania Shilingi Trilioni 16 China yaikopesha Serikali ya Tanzania Shilingi Trilioni 16 Reviewed by Bill Bright Williams on 2:02:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.