Updated Thursday, June 23, 2016

Putin ametoa kipaumbele kwa kujenga SUPER ARMY kuharibu ISISNational Guard force – ambayo ilipitishwa na bunge la Urusi leo-litakuwa chini ya amri ya mtu binafsi mwenye nguvu.
Kikosi hicho kitatumika kwa ajili ya shughuli zote za ugaidi, mahala popote pale duniani na kikiwa na madaraka makubwa,
ikiwa ni pamoja na kuwa na mamlaka ya kupiga risasi katika umati wa watu na kushika watuhumiwa kwa ajili ya mahojiano.

Wataalamu wanasema, kikosi hicho chenye nguvu kitakuwa chini ya rais Putin mwenyewe.

Kitatumika kuendesha shughuli za kijeshi duniani kote,kuwaweka kizuizini watuhumiwa wa ugaidi kwa mda mrefu kabla ya kuwakabidhi kwa polisi.
Kiongozi wa zamani wa KGB ametoa baraka zote kwa bunge la Urusi kwa hiki kikosi maalumu, ambacho kitaongozwa na mmoja 
wa walinzi wake, aitwaye Viktor Zolotov.
Katika mswada huo uliopitishwa katika bunge la Urusi, wabunge 345 wameuhidhinisha huo mpango, wakati wabunge 15 wakipinga
mswada huo.
Rais Putin atakuwa muhusika wa moja kwa moja katika hili jeshi jipya liitwalo ‘super army’
Vita Baridi 2.0: Russia kurejesha mfumo wake wa makombora baada ya Marekani kufanya hivyo.....
Mr Zolotov atakuwa anaripoti moja kwa moja kwa rais wa Urusi,taarifa za kukabiliana na ugaidi na jinsi ya kuwakandamiza 
watu wenye msimamo mkali wa jihadi.
Miongoni mwa nguvu mpya watakazopewa hiki kikosi maalumu ni kupiga risasi katika umati wa watu kama kuna shambulio
la kigaidi au mateka- ambapo kwa sasa njia hii haitumiki kwa sababu za hatari ya kujeruhi au kuua.


Putin ametoa kipaumbele kwa kujenga SUPER ARMY kuharibu ISIS Putin ametoa kipaumbele kwa kujenga SUPER ARMY kuharibu ISIS Reviewed by Bill Bright Williams on 4:44:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.