Updated Monday, June 27, 2016

NATO wameanza mazoezi makali ya kijeshi Ukraine


Wanachama wa NATO, ikiwa pamoja na vikosi kutoka Marekani, wameanza mazoezi makubwa ya kijeshi magharibi ya Ukraine.
Wizara ya ulinzi ya Ukraine inasema, mchezo huu wa kivita ulianza saa 9.00 am siku ya jumatatu katika International Peacekeeping na makao makuu ya usalama(IPSC) huko Yavoriv nchini Ukraine.
Kwa mujibu wa vyanzo vya jeshi, zaidi ya vikosi 2,000 kutoka nchi 14 wanachama wa NATO  na wapenzi wao kutoka mashariki mwa Ulaya watahusika katika hayo mazoezi.
Press TV reports:
Mazoezi haya yatahusisha vifaa vya kijeshi, ikiwa ni pamoja na magari ya kivita, helikopta za kijeshi na ndege.
Awamu ya kwanza ya mazoezi ya kila mwaka ya kijeshi yatamalizika Julai 8.
Katika mazoezi ya mwaka huu, Rapid Trident  itahusisha Ukraine, United States, Belgium, Bulgaria, Canada, Georgia, United Kingdom, Moldova, Lithuania, Norway, Poland, Romania, Sweden na Turkey.
Mapema mwaka huu, NATO walifanya mazoezi ya kijeshi kwa mda wa siku 10, ikihusisha askari 31,000 kutoka Poland na Marekani.
Urusi, ina wasiwasi kwa kuongezeka kwa majeshi ya NATO karibu na mipaka yake,na inatishia kuchukua hatua stahiki kukabiliana na ongezeko la shughuli za kijeshi kutoka nchi za Magharibi.
NATO wameongeza vikosi vyake karibu na mpaka wa Urusi tangu mahusiano na Moscow kudorora  April 2014 kwa kitendo cha Urusi kuchukua Crimea na kufanya moja ya sehemu ya Urusi.
Jimbo la Donetsk mashariki mwa Ukraine lilishuhudia mapigano makali kati ya wanaounga mkono vikosi vya Moscow na Jeshi la Ukraine. 
Marekani na washirika wake wa Ulaya wanailahumu Moscow kwa kuikandamiza Ukraine.Urusi inapinga kuhusika kwenye umwagaji damu na inazilahumu nchi za magharibi kwa kuchochea umwagaji damu ambao mpaka sasa umegharimu maisha ya watu zaidi ya  9,200 na kujeruhi zaidi ya watu  21,000.
Kamanda wa jeshi la Marekani alionya mapema wiki hii kwamba NATO haiwezi kuzuia nguvu ya kijeshi ya Urusi.
Pia kamanda wa majeshi ya ardhini ya Marekani huko Ulaya, Generali Ben Hodges, alisema Vikosi vya Urusi ni rahisi kuteka Estonia, Latvia, and Lithuania “kwa haraka sana kuliko sisi tunavyoweza kufika huko kuvilinda.

NATO wameanza mazoezi makali ya kijeshi Ukraine NATO wameanza mazoezi makali ya kijeshi Ukraine Reviewed by Bill Bright Williams on 8:25:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.