Updated Wednesday, June 29, 2016

Mzee wa miaka 61 apata mpenzi doli (Toy)


Senji Nakajima mwenye umri wa miaka 61, amenunua doli na kulifanya kuwa mke wake wa maisha baada ya kuwa mbali na mkewe aliefunga nae ndoa na kuzaa nae watoto wawili.
Hakika, Senji Nakajima, kwa sasa anajivunia kuwa na mahusiano ya kimapenzi na doli lake analoliita Saori- baada ya kumpenda sana kutoka ndani ya moyo huyo mdoli.
Kwa sasa Senji anasema ana mahusiano na doli hilo kwa mda wa miaka sita, baada ya kuwa mbali na mkewe kwa kipindi chote hicho kutokana na kazi.
Miezi michache iliyopita  Mr Nakajima, kutoka Tokyo Japan, alidai kuwa mahusiano ya wawili hao yapo katika ngazi za juu sana.


Kwa upande wake Senji anadai kupata upendo wa uhakika, na anafurahia sana kuwa na mahusiano na Saori. Wawili hawa wanaishi katika nyumba ya pamoja - na pia wanachangia kitanda kimoja. Na anapenda kumchukua na kwenda nae shopping na kumnunulia nguo.


Mr Nakajima alisema:" Hawezi kumsaliti kamwe mrembo wake"
"Anadai amechoshwa na mahusiano ya binadamu. Wengi wao hawana moyo wa huruma.
"Kwa upande wake Senji Saori ni zaidi ya doli kwake.
Anamsaidia sana mpenzi wake na kufurahia maisha kwa pamoja.


Madoli haya kutoka kwa Wadachi, yanazidi kupata umaarufu Asia ambayo yananunuliwa kwa  £4,000.
Yana midomo mizuri, ngozi ya kuvutia kama ya binadamu wa kawaida- kazi kwako tu kuchagua umbo na rangi ya nywele.


Mzee wa miaka 61 apata mpenzi doli (Toy) Mzee wa miaka 61 apata mpenzi doli (Toy) Reviewed by Bill Bright Williams on 4:24:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.