Updated Thursday, June 30, 2016

Mlipuko waua baada ya mlipuaji wa Taliban kugonga msafara wa polisi.


Kabul, Afghanistan-- Wapiganaji wa Taliban wamefanya mashambulio mawili ya kujitoa muhanga siku ya Alhamisi, wakilenga msafara wa mabasi yaliyokuwa yamebeba polisi, nje kidogo ya mji mkuu na kuua watu 37, wengi wao wakiwa ni polisi,
na kujeruhi 40, mamlaka nchini humo zilisema.
Mashambulio yalifanyika katika wilaya ya Pagham, maili 12 magharibi ya Kabul, kwa mujibu wa Rahmati, gavana wa Paghman.
Mjitoa muhanga wa kwanza alijilipua kati ya mabasi mawili yaliyokuwa yamebeba polisi waliokuwa kwenye mafunzo,
na mshambuliaji wa pili alilenga wale waliokuwa wanakimbilia kwenye eneo la tukio hili watoe msaada na pia shambulio hilo lilipiga gari la tatu, Rahmati alisema. Alisema pia raia wanne ni miongoni mwa waliouawa.
Katika taarifa iliyotolewa alhamisi, Wizara ya mambo ya ndani imesema, polisi 30 walioajiriwa waliuawa na 58 walijeruhiwa.

Taliban wanadai kuhusika na shambulio hilo, baada ya kutuma e-mail kwa Associated Press   kwa msemaji Zabihullah Mujahid.


Mlipuko waua baada ya mlipuaji wa Taliban kugonga msafara wa polisi. Mlipuko waua baada ya mlipuaji wa Taliban kugonga msafara wa polisi. Reviewed by Bill Bright Williams on 9:56:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.