Updated Wednesday, June 29, 2016

Mlipuko uliotokea uwanja wa ndege nchini Uturuki, umerekodiwa kwenye Kamera.


Kamera ya CCTV imeonyesha moja ya mlipuko ambao uligharimu maisha ya watu zaidi ya 30 na kujeruhi wengine 140, nchini Uturuki katika uwanja wa ndege wa Ataturk.

Video inaonyesha mwanga mkali katika msongamano wa watu, ambapo ulifuatiwa na moshi mnene mweusi na kusababisha hofu miongoni mwa abiria.
Mlipuko huu ulitokea siku ya jumanne katika uwanja wa ndege wa kimataifa huko Instanbul.

Onyo video hii inaweza kuwa na maudhui yasiyoridhisha kwa wengine 
Vyombo vya habari nchini Uturuki vinadai kwamba mlipuko huo ni shambulizi la kigaidi na lilikuwa linalenga maeneo mawili tofauti katika uwanja wa ndege.

Onyo video hii inaweza kuwa na maudhui yasiyoridhisha kwa wengine 


Mlipuko uliotokea uwanja wa ndege nchini Uturuki, umerekodiwa kwenye Kamera. Mlipuko uliotokea uwanja wa ndege nchini Uturuki, umerekodiwa kwenye Kamera. Reviewed by Bill Bright Williams on 2:17:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.