Updated Thursday, June 23, 2016

Madaktari wametoa onyo kwa wale wanaotumia smartphone katika giza


LONDON - Onyo: Kutumia smartphone yako wakati umejilaza katika kitanda wakati wa usiku inaweza kudhoofisha havoc katika macho yako.
Watu wawili walipata upofu wa mda mfupi baada ya kuangalia simu zao katika giza, wanasema madaktari ambao kwa sasa wanawatahadharisha wengine kutotenda kitendo hiki.

Cha kufanya: Hakikisha unatumia macho yako yote mawili wakati ukiwa unatumia smartphone yako katika giza.

Alhamisi, New England Journal of Medicine, Madaktari walikuwa wakitoa ufafanuzi wa tukio la wanawake wawili, miaka 22 na 40, ambao walipata upofu wa mda miezi kadhaa iliyopita.
Wanawake hawa walilalamika kwa kupoteza uwezo wa kuona kwa mda wa dakika 15.Walifanyiwa vipimo mbalimbali ikiwa pamoja na MRI scans na vipimo vya moyo. Hata hivyo madaktari hawakuweza kupata kibaya chochote katika miili yao kinacholeta tatizo.

Ila mda mfupi baada ya kwenda kwa wataalamu wa macho, tatizo lao likaweza kugundulika.

"Mimi tu nikawauliza,'Ni nini hasa walikuwa wanafanya wakati tukio hilo linatokea?" Daktari Gordon Plant wa Hospitali ya Moorfield aliwauliza.
Alifafanua ya kwamba wanawake wote kwa kawaida inaonekana wakati wanatumia smartphone zao, wanaangalia kwa jicho moja tu
na huku lingine likiwa limefunikwa na mto wa kulalia.
Kutokana na ufafanuzi wao, daktari alisema,"Basi,wakati unatumia simu yako kwenye giza, jicho moja linakuwa linapata mwanga wa simu na huku jicho lingine likiwa kwenye giza.
Mara baada ya kumaliza kutumia simu, itachukua mda kwa lile jicho lingine ambalo lipo kwenye giza kufanya kazi kama lile
jicho lililoona mwanga wa simu. Alisema Daktari Plant.
Alisema pia upofu wa mda mfupi hauna madhara, na ni rahisi kuuzuia kwa kuepuka kuangalia smartphone yako kwa jicho moja,
mara unapotaka kutumia simu yako kwenye giza, unashauria kutumia macho yote mawili.

Madaktari wametoa onyo kwa wale wanaotumia smartphone katika giza Madaktari wametoa onyo kwa wale wanaotumia smartphone katika giza Reviewed by Bill Bright Williams on 6:49:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.