Updated Monday, June 6, 2016

Israel Wametengeneza Kamera Ya Kugundua Magaidi


Israel wamegundua aina mpya ya kifaa chenye uwezo wa kumtambua gaidi, kwa kuangalia tu uso wake.
Kampuni hii ya Israel inasema technolojia hii ina uwezo wa ku-scan uso wa mtu na moja kwa moja itaeleza wasifu wake wote.

Mintpressnews.com wameripoti hivi:
Wanadai technolojia hii itawezesha makampuni ya usalama kwa kuchunguza na kuwajua magaidi na wahalifu kabla ya kupata nafasi ya kufanya madhara, na kampuni hii tayari imesha-saini mkataba na Idara ya Usalama, kwa mujibu wa Washington Post.The Mirror wameripoti kwamba technolojia hii ilipata ufanisi wa kutambua magaidi 9 kati ya 11 ambao walihusika katika mauaji ya Paris.
“Tunawaelewa binadamu zaidi ya uelewa wa mtu mmoja mmoja", maneno haya alisema mtendaji mkuu a kampuni hii(Faception)
Shai Gilboa."Utu wetu unatambulika kwa DNA zetu na mtazamo katika uso.Ni aina ya ishara"
Faception inatumia classifier 15 ambazo aziwezi kuonekana kwa macho ya binadamu,ikiwa ni pamoja na extrovert, genius, professional poker player, pedophile, na gaidi.
Classifier hii inawakilisha mtu fulani mwenye utu wa kipekee au mkusanyiko wa sifa na tabia.

Israel Wametengeneza Kamera Ya Kugundua Magaidi Israel Wametengeneza Kamera Ya Kugundua Magaidi Reviewed by Bill Bright Williams on 11:55:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.