Updated Friday, May 13, 2016

Utafiti Mpya Unaonyesha Uhusiano Uliopo Kati Ya Simu na Saratani na Mambo mengine kwa Watoto


Kumekuwa na ushahidi mwingi kwa miaka kadhaa sasa,unaoeleza uhusiano wa matumizi ya simu na saratani. Watafiti wa Baltimore wameeleza kwamba kuna ushahidi wa wazi kabisa na watoto wapo kwenye hatari zaidi.
Wataalamu wanasema wazazi na mama wajawazito wanatakiwa kuwa makini zaidi, shirika la Environmental Health Trust wametoa wito kwa wazalishaji wa simu za mkononi kusaidia mfuko wa utafiti wa jinsi ya kutibu na kuzuia madhara yatokanayo na mionzi
CBS Baltimore reports:
Utafiti unaonyesha kwamba simu za mikononi zinaleta matatizo ya afya kwa watoto. Hii ndio sababu inawafanya wataalamu waseme kwa wazazi na mama wajawazito kuwa makini zaidi.
Matumizi ya simu za mkononi ni jambo lililozoeleka katika maisha ya kila siku na utafiti uliofanywa unaonyesha matumizi haya yana madhara kiafya--zaidi kwa watoto na watoto wachanga.

Ushahidi wa swala hili ni dhahiri: simu za mkononi zinasababisha kansa ya ubongo",alisema Dr.Devras Davis, rais katika,Environmental Health Trust.
Dk Davis anasema ubongo wa vijana wadogo unachukua mara mbili zaidi ya mionzi kuliko watu wazima.

Pia  Dr. Hugh Taylor, Yale School of Medicine alisema, "Kuna uhusiano kati ya matumizi ya simu ya mkononi katika mimba na matatizo ya kitabia katika watoto wao,"
Madaktari wanasema ubongo wa mtoto mchanga--hata kama yupo tumboni kwa mama yake-ana hatari ya kudhurikana hii mionzi.
"Weka simu mbali na tumbo - hasa mwishoni mwa ujauzito," alisema Dk Davis.
Wataalamu wanashauri kutumia headsets, kwa simu zao na kama hauna matumizi na simu yako iweke mbali nawe

Utafiti Mpya Unaonyesha Uhusiano Uliopo Kati Ya Simu na Saratani na Mambo mengine kwa Watoto Utafiti Mpya Unaonyesha Uhusiano Uliopo Kati Ya Simu na Saratani na Mambo mengine kwa Watoto Reviewed by Bill Bright Williams on 11:25:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.