Updated Saturday, April 16, 2016

Vitu 7 vya kufanya hili ujilinde na wadukuzi wa mitandaoni (Hackers)


Utumiaji wa Internet huja na hatari zake.Hackers wanaweza kuiba utambulisho wako,kuiacha tupu akaunti yako ya benki au kuweka code za malicious  kwenye kompyuta yako.
Kuja kwa smartphone kwenye soko linafanya uhalifu kwenye mitandao kuongezeka.
Ila kuna vitu 7 vya kufanya hili kuwapa shida hackers kuingia katika device yako.
Ukiangalia hali ya usalama wa internet, Norton security makers symatrec wametoa ripoti ya kina kwa kuchunguza maisha yetu ya digitali.Kampuni iligundua kuwa uvamizi na udhaifu umefikia asilimia 214 ukilinganisha na mwaka 2014.
Hizi ni hatua kadhaa wateja wanaweza kuzichukua ili kulinda data zao, na kuwapa ugumu hackers kuwashambulia

1.Tumia strong password
Symatrec wameshauri kwamba utumiaji wa strong password na kubadilisha password yako mara kwa mara, ni njia mojawapo ya kujilinda dhidi ya hackers.

2.Mitandao ya kijamii: Hackers wanaipenda sana
Hakikisha kwamba unajizuia ku-share taarifa zako binafsi katika mitandao ya kijamii.Taarifa zako binafsi na taarifa kuhusu fedha zako au account yako ya benki usiviweke kwenye mitandao ya kijamii

3.Nunua online kwenye tovuti zinazoaminika
Usiende kununua kitu online kwa kutumia public computer. Tumia device yako binafsi, kama PC yako au smartphone na tablet.

4.Kuwa makini na free public Wi-Fi
Free public Wi-Fi ni nzuri kwa kusoma habari. Ila sio kila mara ni salama kwa kubadilishana taarifa za siri.

5.Update software yako mara kwa mara
Kama uki-install software mpya, hakikisha una-update kwa developer na sio kutumia third party ambazo zinaweza kuja kuficha malware

6.Tumia protection
Computer antivirus software zinapatikana kwa urahisi, inakupasa utumie antivirus kwenye operating system yako.

7.Kuwa makini na fake warning
Zaidi ya mara moja,unaweza kuona alerts imekuja na kusema your computer is infected with some virus.Usiamini maneno hayo.Cha kufanya hakikisha mfumo wako mzima upo protected na tumia antivirus program ku-scan device yako.

Vitu 7 vya kufanya hili ujilinde na wadukuzi wa mitandaoni (Hackers) Vitu 7 vya kufanya hili ujilinde na wadukuzi wa mitandaoni (Hackers) Reviewed by Bill Bright Williams on 10:57:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.