Updated Friday, April 15, 2016

Hakikisha kwamba unatupa mbali hizi bidhaa zinazoua taratibu


Vanilla,chocolate,apple, na mdalasini ni haina mbalimbali za bidhaa za air freshner zenye harufu nzuri.Lakini swali linabakia, je bidhaa hizi ni salama kwa matumizi? Utafiti mpya umethibitisha: Bidhaa hizi ni hatari kwa afya yako!
Matokeo mapya yanaonyesha kwamba baadhi ya bidhaa hizi kama, mishumaa yenye harufu nzuri na kila aina ya air freshners inaweza kuwa hatari kwa afya zetu.
Utafiti unaonyesha kwamba, matumizi ya mda mrefu wa hizi bidhaa itakuletea matatizo ya mapafu na inaweza kusababisha pumu. Na pia kemikali yake ikiingia ndani ya mwili wako inaweza kubadilisha muundo wa DNA yako.
Kama wewe ni mmoja wa watu ambae wanataka kufurahia harufu nzuri kutoka kwa ile mishumaa yenye harufu nzuri, unaweza kushangazwa kwa hili;
Mishumaa hii inaweza kukusababishia carcinogenic mutations of DNA. Kemikali zinazotoka katika hii mishumaa zina uwezo mkubwa wa kuharibu mapafu yako,vile vile hizi scents ni sumu; zaidi ya tumbaku.
Air freshners zinahusishwa na matatizo ya pumu, na pia inaweza kukusababishia matatizo ya homoni.
Utafiti unaonyesha kwamba air freshners zina wingi wa formaldehyde, ambayo inaweza kukusababishia kansa ya koo na pua.
Utafiti uliofanywa na International Magazine of Public Health 2013 ulionyesha kuwa wanawake wajawazito ambao walikuwa wanapendelea air freshners wanajifungua watoto ambao wanakuwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kuja kupata matatizo ya mapafu.
Lakini watengenezaji SC Johnson wanasema air freshner yao aina ya 'Glade' ni salama kwa afya za watu. Nani ana uhakika na hilo? Tafiti nyingi zilizofanywa zinaonya dhidi ya matumizi ya bidhaa hizi.
Utafiti unaonyesha kwamba scent candles zisitumike kwa matumizi ya binadamu kwa kuwa ni hatari kwa afya zetu.
Uamuzi ni wako kama bado unaendelea kununua bidhaa hizi hata kama ni hatari kwa afya yako


Hakikisha kwamba unatupa mbali hizi bidhaa zinazoua taratibu Hakikisha kwamba unatupa mbali hizi bidhaa zinazoua  taratibu Reviewed by Bill Bright Williams on 7:36:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.