Updated Thursday, March 3, 2016

Vitu vibaya sana Vinaweza kutokea mwilini mwako ukitumia mwaka mzima kukaa Angani


Wana anga wawili, mmoja raia wa MAREKANI na mwingine raia wa RUSSIA waliokaa katika anga za juu katika kipindi cha mwaka mmoja wamerejea katika sayari ya dunia
Kipindi cha siku 340 ambacho walikuwa katika anga za juu akikuwa cha furaha na cha mchezo. Miili yetu imeumbwa kwa ajili ya hapa duniani,hatujaumbwa kwa ajili ya sehemu zisizokuwa na nguvu za uwiano.
NASA walifanya hivi kuwaacha kwa mda mrefu angani hili wajue ni madhara gani mtu atayapata akiishi angani kwa mda mrefu.
Lengo lingine la NASA ni kutumia mambo waliojifunza kutoka angani hili waweze kumtuma mtu mwingine aende katika sayari ya Mars, safari itakayochukua mda wa miaka miwili na nusu.


Haya ni madhara utakayopata ukikaa angani mda mrefu


1.Bila mazoezi,utapoteza kiasi cha 12% ya uzito wa mifupa yako

2.Hauna haja ya misuli ukiwa anga za mbali,kwa hiyo misuli yako itasinyaa na kufyonza tishu za ziada

3.Unakuwa katika hali ya kukosa usingizi,wana anga wanalala masaa yasiyozidi 6 kwa sababu angani kuna hali za ajabu

4.Kwa kuwa nguvu za mvutano hazikuvuti kwenda chini, basi mgongo utapanuka na utaongezeka urefu hadi 3%

5.Uwezo wako wa kuona utakuwa katika hatari kutokana na kubadilika kwa pressure katika ubongo

6.Mionzi itakayokuwa inakupata ukiwa nje ya dunia ina uwezekano mkubwa wa kukusababishia kansa

Vitu vibaya sana Vinaweza kutokea mwilini mwako ukitumia mwaka mzima kukaa Angani Vitu vibaya sana Vinaweza kutokea mwilini mwako   ukitumia mwaka mzima kukaa Angani Reviewed by Bill Bright Williams on 1:50:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.