Updated Wednesday, March 9, 2016

Tahadhari:Ukiona aina hii ya Mende Nyumbani kwako uwe Makini


Mende hawa wanaonekana kama hawana madhara, ila wanabeba ugonjwa unaosababishwa na vimelea vya trypanosomes cruzi. Mara nyingi aina hii ya mende wanaonekana sana maeneo ya Marekani na Mexico
Duniani kote kuna watu karibu na milioni 8 wameathirika na hivi vimelea.
Taasisi ya kuzuia na kupambana na magonjwa imeelezea kwamba sio rahisi kwa mende kumpa binadamu ugonjwa huu utokanao na vimelea vya trypanosomes vinavyosababisha ugonjwa ujulikanao kama Chagas. Ugonjwa unaenezwa kwa kile kinyesi chao. Mtu anaweza kupata ugonjwa huu wa chagas pale tu kinyesi cha huyu Mende kitaingia kwenye jeraha lolote au kupitia sehemu yeyote ya mwili ikiwa kwenye mdomo au masikio.
Endapo uking'atwa na huyu mende sehemu iliyong'atwa itaanza kusikia inawasha ukikuna itakuletea kama mikwaruzo,vile akikung'ata ni mwanzo wa kukuletea ugonjwa.Watu waliong'atwa na huyu mende hawajisikii homa yeyote, kwa hiyo hawaendi hospitali. Ila madhara ya huyu mende kwa watu aliowauma asilimia 30 wanaweza wakapata magonjwa ya moyo

Ili kudhibiti Mende huyu asiingie ndani kwako yakupasa;

Uondoe kuni na brashi zilizo karibu na nyumba yako
Ziba nyufa zote katika nyumba yako
Weka maeneo yanayokuzunguka yakiwa safi
Ni vyema kuwa na mnyama mdogo anaelala ndani ya nyumba, hasa wakati wa usiku

Tahadhari:Ukiona aina hii ya Mende Nyumbani kwako uwe Makini Tahadhari:Ukiona aina hii ya Mende Nyumbani kwako uwe   Makini Reviewed by Bill Bright Williams on 11:53:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.