Updated Tuesday, March 8, 2016

Tahadhari, Usitumie simu yako wakati unachaji


Je unatumia smartphone yako huku unachaji,unatakiwa ufikirie mara mbili kabla ya kufanya kitendo hicho.
Gabbie mdada mwenye umri wa miaka 13 alipata majeraha mabaya ya kuungua wakati alivyokuwa anatumia simu yake huku anachaji
Alikuwa anatumia simu aina ya LG d500 huku akiwa ameichomeka kwenye chaji. Alisema alirushwa na umeme ambao ulitoka kwenye simu yake hadi kwenye cheni aliyovaa shingoni na kumsababishia kuungua shingo yake
Alipata majeraha makubwa ya kuungua na sasa shingo yake imebaki na alama za kuungua baada ya kupona majeraha
Kumekuwa na matukio kadhaa katika miaka michache iliyopita ambapo simu za mkononi zimekuwa zikilaumiwa kwa kusababisha majeraha ya shoti za umeme:
Mwaka 2010, toddler kutoka Calorado alipata majeraha mabaya baada ya kuiweka chaji ya simu aina ya apple mdomoni mwake.
Chaji za Usb zilihusishwa na kifo cha mwanamke wa Australia mwaka 2014. Mwanamke huyu alipigwa shoti pale alipokuwa anaongea na simu huku anaichaji

Tahadhari, Usitumie simu yako wakati unachaji Tahadhari, Usitumie simu yako wakati unachaji Reviewed by Bill Bright Williams on 1:59:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.