Updated Monday, March 14, 2016

Kutoka kwa harufu mbaya mdomoni yaweza kuwa ni dalili ya ugonjwa hatari


Kwa miaka mingi, madaktari wamegundua harufu mbaya mdomoni inaweza kuwa ni sababu mojawapo ya magonjwa fulani.
Wazo la kutumia vipimo vya pumzi kama utambuzi wa kitabibu sio mpya, Hippocrates ni mwanafalsafa wa kwanza kutambua harufu ya pumzi inaweza kuhusiana na ugonjwa katika miaka ya 400BC
Katika ripoti iliyotolewa na jarida la wall street journal, madaktari walielezea technolojia ya kuchunguza kemikali zinazopatikana katika pumzi
Kutoka kwa harufu mbaya mdomoni yaweza kuwa ni dalili ya magonjwa yafuatayo;

1.Kisukari
Harufu kama ya matunda inayotoka kwenye kinywa inajulikana kama Ketoacidosis, ni njia ya kawaida inayoonyesha matatizo makubwa ya kisukari

2.Kansa ya mapafu
Technolojia mpya inaweza kugundua kansa ya mapafu kwa kupima kemikali zinazopatikana katika hewa unayoitoa katika kinywa

3.Kushindwa kwa figo
Figo zetu zinahusika kutoa uchafu, kama figo inashindwa basi sumu zitaenea mwilini.Matokeo yake ni uchafu kujijenga zaidi na mwishowe unaingia hadi kwenye mfumo wa upumuaji

4.Obesity
Kituo cha afya cha Cedars-Sinai huko Los Angels waliona kuna uwezekano wa harufu ya hewa ya mtu inaweza kuwa na uhusiano na obesity

5.Kushindwa kwa moyo
Utafiti uliofanywa mwaka 2012 uligundua watu wenye matatizo ya moyo wana harufu tofauti kabisa katika pumzi zao

NB:Maelezo haya hayahusiani na Harufu ya kinywa inayotokana na kutopiga mswaki

Kutoka kwa harufu mbaya mdomoni yaweza kuwa ni dalili ya ugonjwa hatari Kutoka kwa harufu mbaya mdomoni yaweza kuwa ni dalili   ya ugonjwa hatari Reviewed by Bill Bright Williams on 11:24:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.