Updated Tuesday, March 22, 2016

Kinywaji hiki kitaharibu mifupa yako kutoka ndani na kudhuru kila kiungo cha mwili wako


Watu wengi sana duniani wanapendelea kinywaji hiki, bila hata ya kutafakari ni madhara gani yatawapata. 
Nadhani kila mtu anajua utumiaji wa vinywaji vyenye sukari ni hatari kwa afya yako, ila bado watu wengi wa hapa Africa Mashariki wanatumia sana vinywaji hivi. Ebu nikuulize swali, hivi unajua ni jinsi gani unywaji wa soda unaharibu afya yako?

Soda na Osteoporis
Kinywaji cha soda kina phosphoric acid na caffeine. Kutokana na utafiti uliofanywa na Framingham 
Osteoposis mwaka 2006 kwa wanaume na wanawake 2500 uligundua ya kuwa unywaji wa cola wa kila siku utapunguza BMD katika hips za mwanamke, na pia utafiti mwingine umegundua kwamba jambo hili linahusishwa na kuongezeka kwa phosphorus ambayo itazuia unyonywaji wa calcium. Pia wataalamu wa maswala ya afya wanasema asidi ya Phosphorus inatoa ile calcium iliyopo katika mifupa ya binadamu.
Pia wataalamu hawa wanasema utumiaji wa gramu 330 za caffeine, au vikombe vinne vya kahawa kila siku itakuharibia mifupa yako. Hii ni kwa sababu caffeine itaingiliana na ufyonzwaji wa calcium na kusababisha calcium itoke nje kwa njia ya mkojo

Hizi ni sababu nyingine za kuacha kutumia soda
1.Itakuongezea uzito
2.Kuharibu ini
Soda zina kiwango kikubwa cha fructose,ambayo ina madhara katika ini lako kama utatumia kwa kiwango kikubwa.
3.Kuharibu Meno
4.Magonjwa ya figo
5.KisukariKinywaji hiki kitaharibu mifupa yako kutoka ndani na kudhuru kila kiungo cha mwili wako Kinywaji hiki kitaharibu mifupa yako kutoka ndani na   kudhuru kila kiungo cha mwili wako Reviewed by Bill Bright Williams on 2:50:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.