Updated Wednesday, March 9, 2016

Jinsi ya kugundua saratani ya ngozi


Melanoma ni aina ya saratani ambayo ni hatari zaidi kuliko saratani zote za ngozi,ni hatari kwa maana inaweza kuenea mwili mzima
Hapa nitaelezea habari muhimu kuhusu hali hii. Ni vyema kugundua kwamba melanoma ni tatizo kubwa.
Aina mbaya zaidi ya saratani ya ngozi ni Melanoma. Kwa ujumla watu 232,000 wana ugonjwa huu na 55,000 wanakufa kila mwaka kwa ugonjwa huu. New zealand na Australia ndio nchi zinaongoza kwa idadi kubwa ya wagonjwa wa aina hii ya kansa duniani. Hata Ulaya na Marekani kuna wagonjwa wengi, wakati Afica, Asia na Latin America ugonjwa huu haupo sana.
Mara nyingi ugonjwa huu unawapata watu wazee.
Kama ukijulikana mapema ugonjwa huu utafanyiwa upasuaji mdogo kwa asilimia 98 utaweza kupona, lakini ukichelewa kutambulika kama una aina hii ya kansa basi asilimia za kupona zinashuka hadi 17.
Utajuaje kama una Melanoma?
Kwa ushauri nadhani utaweza kuokoa maisha yako,ukiona kitu kisichokuwa cha kawaida kinatokea katika ngozi yako, nenda hospitali kwa uchunguzi zaidi, mara nyingi kansa inaanza kama kidonda kidogo au kitu kisichoisha
Unaweza kupunguza uwezekano wa kutopata Kansa kwa kujiepusha na miale ya jua na kutokaa kwenye jua kali
Jinsi ya kugundua saratani ya ngozi Jinsi ya kugundua saratani ya ngozi Reviewed by Bill Bright Williams on 12:14:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.