Updated Saturday, March 12, 2016

Je unalala na nywele zikiwa na maji?Haya ndio madhara yake


Je ukimaliza kuoga unaenda kulala, unaenda kulala bila kutoa maji katika nywele zako? Kama ndio, 
unatakiwa uichunguze vizuri hiyo tabia maana ina matokeo mabaya
Tabia ya kulala na nywele zikiwa bado zina maji ina madhara kwa afya yako, haya ndio madhara yake;

1.Inaweza kukusababishia maumivu ya kichwa
Tofauti na kulala na nywele zikiwa kavu, ukilala na nywele zikiwa na maji zitakuongezea joto la 
mwili. Kutokana na ubichi wa nywele shuka au mto utapata unyevu, kuongezeka kwa joto la mwili na ule unyevu vitakusababishia maumibu ya kichwa

2.Itakuletea Fangasi
Kwa kiasi kikubwa mito tunayolalia inabeba bacteria wanaotokana na kunyonya jasho, seli za ngozi 
zilizokufa,na mafuta katika miili yetu. Nywele zisizo kauka zitavyonzwa majimaji yaliyo katika nywele na kuyapeleka ndani ya mto, na kutokana na joto,mto utakuwa unazalisha Fangasi

Tatizo ni kwamba asubuhi hatuna desturi ya kwenda kuianika mito yetu ili iwe mikavu,sana sana nyakati za baridi,hii inawasaidia bacteria wawe salama na kuongezeka zaidi

3.Nywele zitakatika
Nywele mbichi ni rahisi kukatika wakati umelala

Kwa ushauri akikisha kabla ujaenda kulala unayatoa maji yote yaliyo katika nywele zako kwa kutumia taulo na kuziacha zikiwa kavu kabisa ndio ulale. na tuwe na mazoea ya kuanika mito tunayolalia mara kwa mara ili kudhibiti uzaaji wa bacteria
Je unalala na nywele zikiwa na maji?Haya ndio madhara yake Je unalala na nywele zikiwa na maji?Haya ndio madhara   yake Reviewed by Bill Bright Williams on 3:56:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.