Updated Thursday, March 24, 2016

Dawa hii ya kutuliza maumivu inaua maelfu kila mwaka


Matumizi ya mda mrefu ya dozi za kutuliza maumivu kama vile ibuprofen au diclofenac ina madhara katika suala la shambulio la moyo kama vile matumizi ya madawa ya Vioxx ambayo yalizuiwa kutumika kutokana na hatari kubwa zilizonazo- Utafiti ulisema

Kuna wakati unaweza kuwa unajisikia vibaya na maumivu katika mwili,kipindi hiki mtu anaanza kutafuta dawa ambayo itamsaidia kuondoa maumivu-badala ya kufikiria njia nzuri ya afya, tunajikuta tunaenda kwenye maduka ya dawa na kununua dawa za kutuliza maumivu bila hata  ya ushauri wowote wa daktari
Unajua nini madhara yake-kama unapenda kutumia dawa za kutuliza maumivu mara kwa mara,sio tu maumivu unayokwenda kuyatuliza

Kama ukitumia dawa inayoitwa Ibuprofen,kama tulivyoielezea, wanasayansi wanaihusisha na 
petrochemical ambayo ni hatari sana kwa kukuletea mashambulio ya moyo au ugonjwa wa moyo na uwezekano mkubwa wa kukusababishia kifo (kama ukitumia pamoja na aspirin),ukitumia dozi mbili kuna madhara makubwa ya afya unayoweza kuyapata;
-Upungufu wa damu
-Uharibifu wa DNA
-Kutosikia vizuri
-Shinikizo la damu
-Vifo kwa kupata mafua
-Kuharibika kwa mimba

Kama Ibuprofen,pia madawa mengine ya NSAIDS(non-steroidal anti-inflammatory drugs) yana matokeo mabaya na yanaweza kukuletea magonjwa ya moyo na vifo

Dawa hii ya kutuliza maumivu inaua maelfu kila mwaka Dawa hii ya kutuliza maumivu inaua maelfu kila mwaka Reviewed by Bill Bright Williams on 9:49:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.