Updated Sunday, March 6, 2016

Dalili za mwanzo za kuharibika kwa Ini na Jinsi ya kuimarisha ini lako


Ini ni moja ya kiungo kikubwa katika mwili wa binadamu, iko katika sehemu ya juu kulia mwa tumbo lako,chini ya mbavu.
Ini lina wajibu mkubwa na umuhimu katika maisha yetu, Inapasa kuweka ini lako katika hali nzuri hili liweze kufanya kazi, pia inatupasa tuwe na ufahamu wa dalili za mwanzo za uharibifu wa Ini.

Ini lina wajibu wa kufanya kazi zifuatazo;

.Linasaidia katika uyeyushwaji wa mafuta
.Linatoa sumu kwenye mwili wako
.Linasaidia kusimamia shughuli za homoni
.Linajenga protini
.Linasaidia uzalishaji wa kemikali muhimu katika digetion

Kila kitu tunachokula lazima kwanza kusindikwa na ini kabla ya kusambazwa katika mwili. Kutokana na ufanyaji kazi wa ini, afya zetu zinategemea na jinsi ini linavyofanya kazi katika kilele chake

Sababu za uharibifu wa Ini

Matatizo ya ini kwa kawaida uanza polepole na kwa miaka mingi, sababu kubwa ya matatizo ya ini ni unywaji pombe wa mda mrefu, sababu nyingine ni;

Virusi mbalimbali
Utapiamlo
Mashambulizi ya baadhi ya dawa
Matumizi ya dawa kupita kiasi
Magonjwa kama Kansa na mafuta katika ini
Kisukali kina ongeza uwezekano wa kupata magonjwa ya ini
Hata uvutaji wa sigara sio tu unaongeza uwezekano wa kupata kansa ya mapafu,bali hata kansa ya ini

Dalili za kuharibika kwa ini

Maumivu yasiyo ya kawaida-hasa maeneo ambayo ini lipo
Unajisikia dhaifu na kuchoka
Kuharisha na rangi ya aja kubwa kubadilika
Manjano(ngozi na macho kuwa njano)
Mkojo wa njano wenye weusi
Kupungua kwa uzito
Kichefuchefu na kutapika
Uwino usio sawa wa homoni, inaweza kusababisha mwanaume kuwa na matiti 
Pia kushindwa kwa ini inaweza kusababisha kuongezeka kwa ute kwenye ubongo na figo kushindwa kufanya kazi

Ni wakati gani yafaa kumuona daktari

Kama utajisikia mchovu na uzito kupungua bila sababu
kama una manjano,homa za mara kwa mara,maumivu yasiyo ya kawaida na kutapika

Ni jinsi gani ya kuimarisha ini lako

Unatakiwa ubadilishe mfumo wa maisha,maisha ya mwenendo mbaya yanatakiwa kuachwa
Kama unatumia pombe kupita kiasi,ni wakati wa kuzuia hiyo hali
Zuia matumizi ya caffeine
Acha kutumia sigara,sigara ina sumu ambayo inaweza kudhuru Ini
Baada ya kutumia pombe na caffeine,kunywa maji mengi hili kuzitoa sumu zote mwilini
Pia unaweza kunywa juisi ya lemoni,inasaidia uyeyushwaji wa chakula
Dalili za mwanzo za kuharibika kwa Ini na Jinsi ya kuimarisha ini lako Dalili za mwanzo za kuharibika kwa Ini na Jinsi ya   kuimarisha ini lako Reviewed by Bill Bright Williams on 7:48:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.