Updated Tuesday, February 23, 2016

Wapinzani nchini Burundi wamekubali kushiriki katika Mazungumzo


Wapinzani nchini Burundi wamekubali kushiriki katika mazungumzo ya kumaliza mgogoro nchini Burundi
Mgogoro huu ulisababishwa na uamuzi wa utata alioufanya raisi Nkurunziza wa kugombea awamu ya tatu, ambapo alishinda katika uchaguzi huo julai mwaka jana.
Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa alisema, Raisi wa Burundi Pierre Nkurunziza na wapinzani wamekubali kukaa meza moja kujadili mzozo unaoikabili nchi yao

Baada ya kukutana na Nkurunziza na wanasiasa wa upinzani, Ban Ki Moon alisema kwamba pande zote wamekubaliana kukaa meza moja ya mazungumzo, na raisi alithibitisha kuwa atashiriki katika mazungumzo hayo ya kisiasa.
Bado haijafahamika kwamba wapinzani wa Nkurunziza ambao wako uhamishoni, baadhi wako jela na wengine wamechukua silaha, watakuwa tayari kufanya mazungumzo

Ban ki Moon alikutana na vyama pinzani siku ya jumatatu usiku kabla ya kukutana na raisi Nkurunziza siku ya jumanne

Wapinzani nchini Burundi wamekubali kushiriki katika Mazungumzo Wapinzani nchini Burundi wamekubali kushiriki katika Mazungumzo Reviewed by Bill Bright Williams on 11:22:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.