Updated Wednesday, February 24, 2016

Wanasayansi waaanza kufanya utafiti wa virusi vya Zika


Timu za wanasayansi wakiwemo waliotoka katika jimbo la Paraeeba lililoathirika zaidi na virusi vya Zika waanza kufanya utafiti
Timu hiyo ya wanasayansi na mawakala wa maswala ya afya walienda kwenye maeneo yaliyoathirika na kuchukua sampuli za damu na kuwahoji akina mama walioathirika na wamama ambao watoto wao walizaliwa na vichwa vidogo

Katika kipindi cha majuma yajayo watakusanya taarifa kutoka kwa mamia ya akina mama katika jimbo hilo la Paraeeba
Baada ya kutangazwa hali ya tahadhari ya kiafya Mkuu wa Shirika la Afya duniani Margaret Chan aliwasili Mjini Brasilia kufuatilia hali ilivyo ambapo alikutana na Rais wa Brazil, DILMA ROUSSEF na kusema kuwa anafurahishwa na namna serikali inavyoshughulikia tatizo hilo na kutaka jamii 
isaidiwe kupambana na mbu anayeeneza Virusi vya Zika.

Wanasayansi waaanza kufanya utafiti wa virusi vya Zika Wanasayansi waaanza kufanya utafiti wa virusi vya   Zika Reviewed by Bill Bright Williams on 10:10:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.