Updated Tuesday, February 23, 2016

Vyakula 4 vinavyoweza kukuletea SarataniNdani ya miaka miwili iliyopita, idadi ya watu wapatao 1.5 million waligundulika na kansa, nadhani ni mda wa kuangalia ni nini tunakula mpaka idadi inakuwa kubwa kiasi hiki cha wagonjwa wapya wa Saratani.
Hii ni orodha ya vyakula 4 vinavyoweza kukuletea uwezekano zaidi wa kupata kansa kama ukiwa unavitumia

1.Matunda yasiyo ya asili
Matunda ambayo siyo ya asili yana madhara kiafya na yanawekwa baadhi ya madawa ya kuulia wadudu kama vile Atrazile,thiodicarb,organophosphates, pamoja na mbolea yenye wingi wa nitrogen

2.Nyanya za Makopo
Vyakula vingi viwekavyo kwenye makopo, tatizo linakuja juu ya yale makopo, makopo yale yametengenezwa na kemikali ijulikanayo kama bispenol-A, or B
Utafiti uliofanywa mwaka 2013 na Chuo cha Taifa cha Sayansi kilionyesha kwamba BPA ina madhara katika ubongo wa panya
Nyanya ni hatari kutokana na wingi wa asidi, ambayo inaweza kusababisha ile BPA kuyeyuka na kuenea ndani ya nyanya zenyewe

3.Chips 
Madhara ya kula chips unaweza usiyaone mapema ila chips ina kiwango kikubwa cha mafuta na calories ambavyo vitakufanya uongezeke uzito. Utafiti uliofanywa na New England Journal of Medicine unaonyesha kwamba ukila kijiko kimoja cha viazi vya kukaanga kwa siku itakuletea wastani wa kuongezeka kwa uzito wa poundi mbili kwa mwaka. Kutokana na wingi wa mafuta chips zitakuzidishia choresterol, zina wingi wa sodium, kwa watu wengi hii ni sababu ya shinikizo 
la damu 
Pia viazi hivi vilivyokaangwa sana ili ziwe chipsi,kutokana na joto jingi vinatengeneza kitu 
kinachoitwa acrylamine,ikijulikana kama carcinogen ambayo pia inapatikana kwenye sigara 

4. Microwave Popcorn
Vile kama vibegi ambavyo vipo kwenye ile microwave ya kutengenezea popcorn, ambavyo unaziweka zile bisi pale, unaweza usijue kama vina madhara kwenye afya yako, leo jua kwamba vina madhara.Vile vibegi vina kemikali ijulikanayo kama perfluorooctanoic (PFOA).Baada ya kupata moto,kemikali hii inaweza kusababisha utasa na saratani kwa wanyama wa maabara

Vyakula 4 vinavyoweza kukuletea Saratani Vyakula 4 vinavyoweza kukuletea Saratani Reviewed by Bill Bright Williams on 3:11:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.