Updated Monday, February 22, 2016

Vifo kutokana na kimbunga huko Fiji vyaongezekaWELLINGTON, New Zealand - Watu kumi zaidi wamekufa katika kisiwa cha Fiji kutokana kimbunga chenye nguvu kupiga katika kisiwa hicho, mamlaka zinasema 

Msemaji wa serikali Ewan Perrin alisema vifo katika kisiwa cha Koro kimepanda mara mbili zaidi na majengo mengi yameharibiwa
Alisema timu ya watu 30 wameshafika katika kisiwa hicho na wameanza kusambaza vifaa vya tiba, vyakula na maji,na watu watasaidiwa kujengewa makazi ya mda mfupi kwa ajili ya wakazi 4,500 waliopoteza nyumba zao.

Kiongozi huyo alisema,pia wana hofu kuhusu kisiwa cha Taveuni, chenye wakazi wapatao 12,000, kwa maana upataji wa taarifa kutoka kisiwa hicho ni mdogo sana

Kimbunga chenye kasi ya 177miles kwa saa kilipiga kisiwa cha Fiji siku ya jumamosi na kufanya kuwa ni kimbunga kikubwa kupata kupiga Fiji
Vifo kutokana na kimbunga huko Fiji vyaongezeka Vifo kutokana na kimbunga huko Fiji vyaongezeka Reviewed by Bill Bright Williams on 10:33:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.