Updated Sunday, February 21, 2016

Mtoto wa miaka 8 afa mikononi mwa mmewe mwenye miaka 40


Bibi harusi mwenye miaka nane amekufa huko Yemen katika usiku wa harusi yake baada ya kupata majeraha ya ndani kutokana na mapenzi aliyokuwa anapewa na mmewe huyo. Shirika la haki za binadamu limetoa wito wa mwanaume huyo kukamatwa ambaye alikuwa mara tano zaidi ya umri mtoto huyo.

Al Nahar,Lebanon,  alitoa taarifa kwamba kifo hicho kilitokea katika eneo la kabila la Hardh huko 
kaskazini magharibi mwa Yemen, karibu na mpaka wa Saudi Arabia.
kwa mujibu wa shirika la umoja wa mataifa linaloshurikia idadi ya watu (UNFPA), kati ya mwaka 
2011 hadi 2020,wasichana zaidi ya milioni 140 wanatarajiwa kuw ma-bibi harusi. Aidha, wasichana 
milioni 140 kuolewa kabla ya umri wa miaka 18, milioni 50 itakuwa chini ya umri wa miaka 15

Inasemekana kuwa zaidi ya robo ya wasichana wadogo nchini Yemen wanaolewa katika umri usiozidi miaka 15, sio tu wasichana hao wanakabiliwa na matatizo ya kupata afya na elimu bora, pia wanaharusi hao wanakabiliwa na unyanyasaji wa kimwili, kihisia na kijinsia katika hizo ndoa za kulazimishwa.

Mtoto wa miaka 8 afa mikononi mwa mmewe mwenye miaka 40 Mtoto wa miaka 8 afa mikononi mwa mmewe mwenye miaka  40 Reviewed by Bill Bright Williams on 7:04:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.