Updated Monday, February 29, 2016

Milipuko yaua nchini Urusi


Milipuko mitatu ya gesi kwa siku tatu mfululizo katika mgodi wa Grand Nord nchini Urusi imeua watu 36.
Hii ni ajali nyingine kubwa kuripotiwa mchini humo, kulinganisha na ajali ziliyowahi kutokea katika mgodi wa Severnaya katika Jamhuri ya Komi, mnamo mwaka 2010.
Siku ya Alhamisi, ilitokea milipuko miwili katika mgodi huo, karibu na mji wa VORKUTA, na kusababisha vifo vya watu wanne, huku wachimbaji 26 wakitoweka kabla ya miili yao kuonekana, na kuripotiwa kwamba wamefariki.
Hapo jana jumapili, mlipuko mwingine wa gesi umeripotiwa kutokea, ambapo umesababisha vifo vya watu sita, ikiwa ni pamoja na maafisa watano wa Idara ya huduma za dharura, wakati ambapo watu 77 walikuwa chini ya mgodi huo.

  
Milipuko yaua nchini Urusi Milipuko yaua nchini Urusi Reviewed by Bill Bright Williams on 9:45:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.