Updated Saturday, February 20, 2016

Mastaa 5 waliojiharibu wenyewe sura zao


Mara zote watu maarufu wanapenda waonekana kwenye ule muonekano mzuri zaidi, wawe wanavutia zaidi kwenye camera, kila waendapo na wanapenda sura zao zionekane na muonekano mzuri zaidi, Ila kwa bahati mbaya wengine wanapenda kwenda hadi mahospitalini japo tu madaktari wawachonge sura zao wawe na muonekano mzuri kupitiliza

Hawa ni mastaa 10 ambao walijaribu kufanya plastic surgery na mwishowe zikagoma,wakawa na muonekano wa kutisha zaidi badala ya muonekano wa kuvutia zaidi.

5.Amanda Lepore
Kitendo cha kwenda kuchonga sura ili uweze kuuza mtaani si jambo la kiungwana, na wale wafanyao hivyo basi wamejitoa muhanga, liwalo na liwe, Amanda alikuwa mzuri na mdomo wake ulikuwa wa 
kuvutia, na sasa muone alivyo na mdomo wake umezidi upande mmoja


4. Michaela Romanini
Botox na sindano ya kwenye lips ni kama dakika 30 tu kukamilisha vyote. Botox ni sumu ambayo inaufanya uso wako u-paralyze ndio Muitalia Michaela alichofanya, alitumia Botox na sindano na sasa yupo kama alivyo, ule uzuri wake wote umeenda na maji


3.Pete Burns
Pete Burns kutoka bendi ya "Dead or Alive"nae alivutiwa na urembo wa kuchonga, akaenda na akapata daktari sahihi wa kile alichokuwa anataka.2.Donatella Versace
Cheki uso wake sasa,Donatella anaulilia uzuri wake wa asili, aliruhusu kisu kipite kwenye uso wake na sasa yupo tofauti na matarajio yake


1.Hang Mioku
Utabaki bila jibu, dada alivyokuwa mzuri hapo awali,mwenye sura na macho ya kuvutia,ila sasa kawa tofauti sana mara baada ya kufanyiwa plastic surgery,sio kwamba ananenepa la hasha sura yake hiyo inatuna na kuvimba.


Napenda kwa wale wenye mawazo ya kuwa na (baby face) ili ni somo tosha,jikubali jinsi 
ulivyo,usikubali kushawishika,baadae ni madhara makubwa.Mastaa 5 waliojiharibu wenyewe sura zao Mastaa 5 waliojiharibu wenyewe sura zao Reviewed by Bill Bright Williams on 6:05:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.