Updated Tuesday, February 23, 2016

Marekani na Urusi zakubaliana kusitisha mapigano nchini SyriaMakubaliano hayo kati ya Urusi na Marekani yataanza rasmi tarehe 27/02/2016
Kundi kuu la upinzani nchini Syria limesema linaunga mkono makubaliano hayo kwa masharti kwamba miji isizingirwe, wafungwa waachiwe huru na mashambulizi ya mabomu zidi ya raia yasitishwe na misaada ya kibinadamu iruhusiwe

Makubaliano hayo yalijadiliwa kwa njia ya simu kati ya raisi wa Marekani na raisi wa Urusi.
Raisi Vladimir putin wa Urusi  ameyaeleza makubaliano hayo kuwa ni hatua nzuri zaidi kuelekea kusitishwa kwa umwagaji damu na ni mfano wa kuigwa dhidi ya ugaidi

Katibu mkuu wa Umoja wa Mtaifa Bwana Ban Ki Moon amesema makubaliano hayo ni ishara ya matumaini na amezitaka pande zote husika kuheshimu makubaliano hayo

Marekani na Urusi zakubaliana kusitisha mapigano nchini Syria Marekani na Urusi zakubaliana kusitisha mapigano nchini Syria Reviewed by Bill Bright Williams on 9:49:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.