Updated Saturday, February 20, 2016

Maneno ya Manny Pacquiao yafanya mkataba wake na Nike usitishwe


Wadhamini wakubwa wa nguo za michezo Nike wamesitisha mkataba na mcheza masumbwi wa kifilipino Manny Pacquiao baada ya, kuwafananisha wapenzi wa jinsia moja kama watu wasio na thamani zaidi ya wanyama.

Kauli hiyo ya Pacquiao aliitoa wakati alipokuwa akifanyiwa mahojiano kwenye runinga na baadaye katika akaunti yake ya Instagram akaitetea kauli hiyo kwa kusema kwamba alikuwa akisema ukweli kwa muujibu wa kilichoandikwa kwenye Biblia takatifu.

Kampuni ya Nike imetoa tamko lake kwa kusema kuwa kauli ya Manny Pacquiao ni yenye ufinyu wa mawazo.
Kampuni hiyo inayojishughulisha na vifaa vya michezo ikaongeza kusema kwamba inavunja uhusiano na mkata na Manny Pacquiao.

Maneno ya Manny Pacquiao yafanya mkataba wake na Nike usitishwe Maneno ya Manny Pacquiao yafanya mkataba wake na Nike   usitishwe Reviewed by Bill Bright Williams on 6:20:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.