Updated Tuesday, February 23, 2016

Magari 10 yenye nguvu zaidi sokoni

Kila mtu anapenda kitu chochote chenye uwezo mkubwa zaidi,hata kwenye magari mtu anapenda awe na gari lenye nguvu zaidi,haya ndio magari 10 yenye uwezo mkubwa zaidi kuliko magari mengine katika soko la sasa

1. BUGATTI VEYRON 16.4 SUPER SPORT
Injini yenye 1200 horsepower,Veyron Super Sport litakuwa linayapita magari mengine barabarani yaani kama yanatembea kwa mguu vile au kama duma akimkimbiza Kondoo vile. Ni gari lenye spidi ya 252.97miles kwa saa na matairi yake yanapatikana sokoni kwa $70,000
2. FERRARI LAFERARRI
Mara nyingine linajulikana kama F150, Ferrari's LaFerarri injini yake inaweza kutumia petrol au 
umeme. Injini yake ina 950 horsepower,na lina spidi ya 186miles kwa saa
3. MCLAREN P1
Ni gari linalotumia umeme, Injini yake ina horsepower 903, P1 lina spidi ya  217miles kwa saa,ukitoa kiviza chake(inhibitor) spidi inaweza kuzidi zaidi ya hiyo4. PORSCHE 918 SPYDER
Injini yake ina horsepower 795,linaweza kwenda spidi ya 60miles kwa mda wa sekunde 2.2 au 100miles kwa sekunde 4.9.Gari ili linauzwa $845,000

5. FERRARI F12 BERLINETTA
F12 Berlinetta injini yake ina horse power 730. Spidi yake ni 220miles kwa saa na linaweza kutoka spidi 0-60 kwa sekunde 3.1
6. DODGE CHARGER SRT HELLCAT
Injini yake ina 707 horsepower,lina spidi ya 204miles kwa saa. Linaweza kufika spidi ya 60miles kwa mda wa sekunde3.7, na bei zake zipo chini ukilinganisha na magari mengine, bei yake inaanza kwa $59,9957. LAMBORGHINI AVENTADOR LP700
Gari hili injini yake ina horsepower 690. Na spidi yake ni 217miles kwa saa


8. FERRARI FF
Injini yake ina horsepower 651,na spidi yake ni 208miles kwa saa. Ferrari FF linapatikana kwa $300,000
9. MCLAREN 650S
McLaren 650S likijulikana pia kama spider lina milango miwili,na injini yake ina horsepower 641.Linaweza kufika spidi ya 62miles kwa saa kwa dakika 3 na pia linaweza kufika spidi ya 124miles/hr kwa sekunde 8.410. SRT VIPER
Injini yake ina horsepower 640 na spidi yake ni 206miles kwa saaMagari 10 yenye nguvu zaidi sokoni Magari 10 yenye nguvu zaidi sokoni Reviewed by Bill Bright Williams on 9:48:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.