Updated Sunday, February 21, 2016

Karibu watu 130 wamekufa katika mfululizo wa mabomu nchini SyriaDAMASCUS- Karibu ya watu 130 wamekufa jumapili kutokana na mfululizo wa mabomu nchini Syria. Mashambulizi hayo yalifanyika katika vitongoji katika miji ya Damascus na Homs wakati ambao John Kerry alipotangaza hatua za awali za kusitisha mapigano.

Mapema jana mchana, mlipuko ulitokea katika magari mawili maeneo ya makazi katika mji wa Homs. Hili ni eneo linalomilikiwa na vikosi vya serikali, walipuaji ni wanayoipinga serikali ya Assad na Isis wamesema wanahusika na mashambulizi hayo.

Baada ya masaa kadhaa kupita katika miji ya Damascus, mabomu yaliripuka. Isis pia imesema ilihusika kuyatega mabomu hayo.
Ijumaa ndio siku iliyopendekezwa na Marekani na Urusi kusitisha mapigano-lakini mapigano yaliendelea kama kawaida

Ingawa pande zote mbili zinasema bado zipo tayari kufanya mazungumzo
Mwishoni mwa juma Rais Bashar al-Assad alisema hadharani katika mahojiano,'hasa na wao wapo tayari kufanya mazungumzo'
Lakini yeye hana imani na wapinzani wake kuweka silaha chini

Katika mji mkubwa wa Aleppo nchini Syria, ndege za Urusi na jeshi la Syria wanafanya mashambulizi ya pamoja kusambaratisha wapinzani wao. Labda wataweza kupata suluhu, Raisi Obama na Raisi wa Urusi Vladimir Putin watakutana siku zijazo kuongelea juu ya mzozo wa Syria

Karibu watu 130 wamekufa katika mfululizo wa mabomu nchini Syria Karibu watu 130 wamekufa katika mfululizo wa mabomu nchini Syria Reviewed by Bill Bright Williams on 8:52:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.