Updated Saturday, February 20, 2016

Jinsi ya kuondoa nywele zisizohitajika usoni


Wanawake wengi wamekuwa wakitumia njia za gharama kubwa ili waweza kuondoa nywele usoni, sio tu njia hizo zina gharama, pia zinaweza kuwaletea maumivu kwenye ngozi zao,njia ya kutumia laser ni nzuri ila unaweza kupata madhara siku zijazo.

Kuna njia nzuri na za asili za kuweza kukuondolea nywele usizozihitaji usoni mwako,njia hizi hazina gharama kubwa na zitakuondolea moja kwa moja nywele usizozihitaji usoni mwako;
chagua njia mojawapo kati ya hizi;

                                    BAKING SODA

Haya matibabu inakupasa uyafanye kabla ya kwenda kulala, chukua kijiko kimoja cha baking soda, 200ml za maji ya moto,changanya kwa pamoja na acha kwa mda maji yapate uvuguvugu. chukua kipande cha pamba au kitambaa na kiloweke ndani ya mchanyanyiko huo,kikamue kidogo na 
kiweke sehemu ambayo hautaki tena nywele ziote,kifunge ujuavyo na kiache usiku kucha sehemu 
hiyo
Ikifika asubuhi unaweza kuondoa hicho kitambaaa na usisahau kupaka cream yeyote yenye kiini lishe kwa ngozi yako eneo hilo lenye tatizo
Ukirudia mara 2-3 utaanza kuona nywele zinatoka
     
                                 PHARMACY IODINE

Kuandaa haya matibabu yakupasa uwe na 40ml za pombe yenye kiwango cha asilimia 70, 1.5 ya ammonium,2ml za iodine,10ml za castor oil na hydroxide(10%)
changanya kwa umakini mchanganyiko huu mpaka uone unakuwa kama maji(colorless)
Huu mchanganyiko inakupasa kupaka kwenye eneo lenye hizo nywele asubuhi na jioni,matokeo utaanza kuona baada siku chache za matumizi kupita, huu mchanyanyiko utakuondolea moja kwa moja nywele usizozihitaji usoni mwako

                                       NETTLE OIL
Mchanganyiko huu ulikuwa unatumiwa na warembo wengi toka karne ya 17; chukua vijiko vitatu vya nettle oil,changanya na 100ml za vegetable oil, Weka sehemu yenye ubaridi wa kawaida na acha kwa mda wa wiki mbili
Baada ya hapo ichukue na iweke kwenye chupa na ifunike,na uwe unachukua kitambaa au pamba kila jioni ichanganye na hiyo dawa na paka sehemu yenye matatizo, acha kwa nusu saa, na baada ya nusu saa osha uso wako na maji ya uvuguvugu
Njia hii ni tofauti kwa kila mwanamke, fanya hivi mpaka nywele zote ziishe

                        GARLIC/KITUNGUU SWAHUMU

Sugua sehemu yenye tatizo,kwa juisi ya vitunguu swahumu,mara chache katika siku
Acha hiyo juisi ya vitunguu swahumu kwenye uso wako kwa mda wa nusu saa, ili upate matokeo mazuri,Baada ya hapo safisha uso wako vizuri kwa maji ya uvuguvugu, na usisahau kupaka cream yenye virutubisho kwa ngozi yako

Jinsi ya kuondoa nywele zisizohitajika usoni Jinsi ya kuondoa nywele zisizohitajika usoni Reviewed by Bill Bright Williams on 6:14:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.