Updated Tuesday, February 16, 2016

Gari la Google linalojiendesha lenyewe kuruhusiwa barabaraniMnamo mwaka 2009,Google walianza mradi wa kutengeneza magari ya kujiendesha yenyewe.
Mfumo huu wa magari ya kujiendesha yenyewe huenda ukaidhinishwa na kuwa sawa na gari linaloendeshwa na dereva.

Shirika la usimamizi wa barabara kuu nchini Marekani ,ambalo hubuni sheria na utaratibu katika barabara za Marekani lilitoa wazo lake katika barua kwa kampuni ya Google uliowekwa wazi wiki hii.

Hadi kufikia sasa, gari lolote lisilo na dereva halikuweza kuidhinishwa kama linaloweza kuendeshwa 
barabarani.Lakini kutokana na maendeleo ya kiteknolojia,shirika hilo limebadili maono yake.
Hii inamaanisha kwamba teknolojia ya gari la kujiendesha ,ambayo haina udhibiti wa gari hilo kama katika magari mengine ni hatua moja muhimu ya kuruhusiwa katika barabara za hadhara.
Huku Shirika hilo likitoa baraka zake kwa gari hilo ,gari hilo sasa limeafiki mahitaji ya usalama wa magari nchini humo.
Gari la Google linalojiendesha lenyewe kuruhusiwa barabarani Gari la Google linalojiendesha lenyewe kuruhusiwa   barabarani Reviewed by Bill Bright Williams on 2:15:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.