Updated Saturday, February 27, 2016

Faida ya Kunywa Maji kabla ya Kula Chochote


Miili yetu ina uwitaji mkubwa sana wa maji:75% ya maji yanahitajika katika misuli, asilimia 90 ya maji yanahitajika kwenye ubongo, asilimia 22 kwenye mifupa na asilimia 83 ya damu ni maji.Ukielewa hivi basi utajua ni jinsi gani ilivyo na umuhimu wa kunywa maji kila siku katika miili yetu kwa ajili ya afya njema na kuilinda miili yetu dhidi ya magonjwa mbalimbali.
Pendelea kunywa maji glasi 1-4 kwenye tumbo tupu,kabla haujala kitu chochote.
Na haya ndio matokeo yake

1.Ukinywa glasi 1 au 2 za maji kabla ya kifungua kinywa ni njia nzuri ya kutoa sumu na vimelea visivyohitajika  katika miili yetu. Pia maji yana uwezo wa kuzuia magonjwa katika miili yetu

2.Wakati wa usiku miili yetu inafanya marekebisho ya seli na kujisafisha,kwa hiyo ukiamka asubuhi ni vizuri kunywa maji kabla ya kula chochote ili zile seli zilizokufa na uchafu mwingine wowote upate kutoka kwa njia ya mkojo

3.Unywaji wa maji kabla ya chochote inaweza kukupunguzia madhara kwa wale wanaotumia pombe,tumbaku na vyakula vyenye uchafu 

4.Maji yana ushirika mkubwa kwa ngozi na ina manufaa sana kwa afya yako; Kunywa vikombe viwili vya maji kabla ya kula chochote itakusaidia kudumisha ngozi yako na kuzuia makunyanzi katika ngozi yako

5.Ukinywa glasi 2-3 za maji kabla ya kula chochote ni njia nzuri ya kupunguza uzitoFaida ya Kunywa Maji kabla ya Kula Chochote Faida ya Kunywa Maji kabla ya Kula Chochote Reviewed by Bill Bright Williams on 8:07:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.