Updated Sunday, February 28, 2016

Asilimia 80 ya mashambulizi ya moyo yanaweza kuepukwa


Magonjwa ya moyo yanahusika na 1/3 ya vifo vyote duniani. Watu wapatao milion 17 walipatikana na magonjwa mbalimbali ya moyo mwaka jana. Ripoti inaeleza ifikapo mwaka 2030 watu milioni 23.6 watakuwa na matatizo ya moyo

Sababu na dalili za ugonjwa wa moyo
Mshtuko wa moyo hutokea wakati ambapo moja au zaidi ya mishipa ya moyo imeziba.Inaanza polepole mishipa ya moyo inaanza kujenga vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na choresterol. Hali hii inajulikana kama ugonjwa wa ateri, husababisha mashambulizi zaidi ya moyo

Sababu nyingine ya shambulizi la moyo ni kusinyaa kwa ateri ambapo inasababisha damu isiweze kupita kwenda kwenye misuli ya moyo. Matumizi ya tumbaku na dawa za kulevya kama vile cocaine yanaweza kutishia utendaji kazi wa ateri.
Sasa tufanyaje hili kuzuia magonjwa ya moyo?Habari njema ni kwamba asilimia 79 hadi 90 ya mashambulizi ya moyo yanaweza kuepukika
Utafiti ulifanyika katika taasisi ya karolinsa uligundua kwamba ukijijengea tabia zifuatazo katika 
maisha yako utakuwa na afya njema na kuzuia asilimia zaidi ya 80 ya matatizo ya moyo;

1.Chakula chenye afya
2.Usivute sigara
3.Tumia pombe kwa wastani
4.Kuwa na utaratibu wa kucheki afya yako
5.Fanya mazoezi


Asilimia 80 ya mashambulizi ya moyo yanaweza kuepukwa Asilimia 80 ya mashambulizi ya moyo yanaweza kuepukwa Reviewed by Bill Bright Williams on 10:04:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.